Skip to main content

A Prayer of AIM for Monastic Life

Benedict and ScholasticaEe Mungu Mpendwa
tunaomba baraka zako
kwa wamonaki wote, wanaume na wanaweke,
hasa wale wanaoishi na kufanya kazi
katika nchi fukara zaidi za ulimwengu wa tatu.

Utuwezeshe wamonaki wote kuwa watu
wa sala na amani.

Tuwe ishara ya ulimwengu kwa watu wote
ili tuweze kuishi pamoja katika upendo wa Mungu.

Utupe roho pana ya kuwakaribisha wasafiri, watu
masikini waliotupwa na jamaa zao na majirani zetu.

Utufanye tuweze kuwasikiliza na kufunzwa na wale
tunaowahudumia, hasa wale walio fukara zaidi.

Mashirika yetu yawe mhudumu mwenye busara wa
kazi ya kuheshimiwa na ya pumziko takatifu.

Pia kazi iwe ya heshima kwa kila kiumbe kinachoishi, na
hasa ikutukuze wewe Ee Mungu, ili maisha yetu yawe ya
kushuhudia haki za binadamu, huruma na tumaini kwa
wote. Amina.

 

CLICK HERE to request a prayer card.

Read in: Spanish | French | Swahili | Portuguese | Polish | English